Header Ads

Header ADS

Shilole "Wewe Ndio Mwanaume Halisi Sitaki Tena Wakina Uchebe Wapiga Danadana"


Penzi lililofufuka upya kati ya msanii @officialshilole na mpenzi wake rommy3d ambaye ni majasiriamali, akiwa pia ndie mpiga picha wake, limezidi kukolea kiasi cha #Shilole kuamua kumuandikia ujumbe mzito mpenzi wake huyo ambae leo anashaherekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.


#Shilole ambaye ametwaa tuzo ya mjasiriamali bora wa kike wa mwaka kidijitali kwenye Tuzo za Kidijitali (Tanzania Digital Awards) mwaka 2020, ikumbukwe kuwa yeye na mpenzi wake huyo waliwahi kuwa kwenye mahusiano zaidi ya miaka 10 iliyopita kabla ya kuachana kwa sababu ya harakati za kimaisha na mwaka huu wamerejea penzini baada ya wote wawili kutemana na ndoa zao.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram, #Shilole ameandika, "Laiti ningejua kuwa ningekutana na huyu kaka tena (my photographer) ningekaa na kumsubiri na nisingepita kwenye mikono ya waliopiga danadana moyo wangu na kunichukulia poa. Ninaomba nikiri umenifanya nijione mpya wewe ni TAFSIRI halisi ya mwanaume.


"Macho yangu yalifumba kutolijua hili mapema ingawa juhudi zako kimapenzi kwako zilikuwa bayana mnoo, wanasema MUDA huamua na angalia nguvu ya sumaku la penzi lako limenisaka na kunirejesha tena himayani kwako.


"Naomba nikiri kuwa sitaki mwingine tena zaidi yako acha tujiishi na tujifurahie bahati nzuri tuna nguvu ya kutafuta na kila mtu ana security na KIPATO chake. Hata ULIMWENGU upinduke sitapepesa macho yangu wala kufikiria mara mbili bado nitakuchagua wewe ROMY my photographer....!!!' alimalizia msanii @officialshilole.



No comments

Powered by Blogger.