Piere Liquid Ashindwa Kuchagua kati ya Pombe na mke
Mchekeshaji Piere Likwidi amesema hawezi kuacha kunywa bia kwa sababu watu wengi wamemjua kwa 'style' hiyo ya unywaji ila endapo itatokea mke wake atamkataza basi atajaribu kumsikiliza ili kuona kama itawezekana.
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Piere Likwidi amesema hawezi kuacha pombe kwani hajizamletea madhara yoyote ila kama mke wake akimkataza atapunguza kunywa ila sio kuacha kabisa.
"Kusema ukweli mimi siwezi kuacha kwa sababu hivi vitu mimi havijaniletea madhara yoyote ya kunidhuru au kuniathiri na watu wengi wamenifahamu kupitia hivyo, kama mke wangu hapendi nitapunguza kunywa na nitamsiliza kwani ndani ya nyumba kunahitajika maelewano na makubaliano ili kufikia muafaka" amesema Piere Likwidi
Aidha Piere Likwidi ameongeza kusema bado hajajaliwa kupata mke ila ana mwanamke ambaye anaishi naye na wana muda wa mwaka mmoja mpaka sasa.
No comments