Kaze: Yanga Tulieni, Mambo Bado
BAADA ya kufanikiwa kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kileleni, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amefunguka kuwa matokeo ya kumaliza mzunguko wa kwanza kwa kuwa kileleni yanawapa chachu ya kuweza kuendeleza wimbi la ushindi katika mzunguko wa pili.
Yanga wamefanikiwa kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa vinara wa ligi, wamepata pointi 43 kupitia michezo 17, wameshinda 13 na wametoa sare nne huku wakiwa hawajapoteza mchezo wowote.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Kaze alisema, amefurahishwa na matokeo ya ushindi dhidi ya Ihefu kwa ushindi wa mabao 3-0 na kudai kuwa kujitoa kwa wachezaji ndio kumesababisha wapate alama tatu.“
Tunashukuru kuweza kumaliza mzunguko wa kwanza tukiwa tunaongoza msimamo wa ligi, hii ni kutokana na wachezaji kujitoa na kujitambua kuhakikisha tunapata pointi tatu katika kila mchezo ambazo zimetufikisha hapa.“
Ni matumaini yetu tutaanza vyema mzunguko wa pili ili tuweze kufanikiwa kufanya vizuri ili mwisho wa siku tuweze kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi,” alisema Kaze
Stori: KHADIJA MNGWAI, Dar es salaam
No comments