JAMAA WA KUSAMBAZA PICHA CHAFU Za ‘Ngono’ Kwa WhatsApp Anaswa
Mfanyabiashara, Faraji Omary (26) Mkazi wa Mbagala Jijini Dar es Salaam akiwa amefunika uso kukwepe kamera za mapaparazi waliokuwa wakitekeleza majuku yao.
Mfanyabiashara, Faraji Omary (26) Mkazi wa Mbagala Jijini Dar es Salaam amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kusambaza picha chafu za ngono kwa njia ya Whatsapp kinyume na sheria ya makosa ya kimtandao.
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali, Adolf Ulaya amesema kuwa mshtakiwa Omary akiwa eneo la kariakoo Wilaya Ilala jijini Dar es Salaam, mnamo Desemba 4,2020 alisambaza picha chafu za ngono kwa njia ya Whatsapp kinyume cha sheria ya makosa ya kimtandao.
Miongoni mwa mashtaka hayo manne Katika mshtakiwa Omary akiwa eneo la Kariakoo Wilaya ya Ilala mnamo Desemba 10,2020 alitengeneza tiketi zenye maneno machafu aliyokusudia kusambaza kwa kuziuza zenye maudhui Machafu kwa jamii kinyume cha sheria.
Baada ya kusomewa mashataka hayo mshtakiwa amekatana kutenda makosa hayo na hakimu aliyesiliza Shauri hilo, Hakimu Mkazi mwandamizi, Rashid Chaungu amesema mshtakiwa dhamana ipo wazi ambapo wadhamini wametakiwa kuwa wawili ambao watasaini bondi ya Mil 5 kila mmoja na barua za utambulisho.
Mshtakiwa Omary ameshindwa kutimiza masharti hayo na amepelekwa Segerea hadi kesi itakapotajwa tena Januari 11, 2021.
No comments