Huyu Hapa Jambazi Aliyefariki Akifanyiwa Upasuaji wa Kubadili Sura
ANAFAHAMIKA Kwa jina la Amado Carrillo Fuentes, alizaliwa Desemba 17, 1956 huko Sinaloa, Guamuchil nchini Mexico na anafahamika zaidi kama "The Lord of the Skies" na hiyo ni kutokana na kasi aliyokuwa nayo katika biashara haramu ya uuzaji wa dawa za kulevya nchini Mexico na kumpa umaarufu pamoja na kuufikia utajiri kwa kumiliki dola za kimarekani zipatazo bilioni 25.
Amado alimiliki ndege nyingi binafsi ambazo alizitumia kusafirisha dawa za kulevya duniani kote, imeelezwa kuwa alimiliki ndege nyingi zikiwemo Boeing 30.
Imeelezwa kuwa Amado alilelewa na mjomba wake na ndiko alipoanza kujifunza kuuza dawa za kulevya, alifundishwa namna ya kusafirisha dawa za kulevya kutoka kundi la Guadalajara Cartel lililoongozwa na mjomba wake na baadaye akaja kuwa msimamizi mkuu wa genge la Juarez Cartel na hiyo ni baada ya kumuua rafiki yake na aliyekuwa bosi wa genge hilo Rafael Guajardo.
Licha ya kumiliki ndege nyingi binafsi imeelezwa kuwa pia alimiliki silaha za kivita na baadaye alitanua biashara yake katika nchi kubwa ikiwemo Marekani.
Anguko la Amado lilikuwa la aina yake hasa pale alipoanza kutafutwa na mamlaka za usalama kutoka Marekani na Mexico, aliamua kufanya upasuaji wa kubadilisha mwonekano wake mwaka 1977 ili aweze kukwepa mkono wa dola lakini upasuaji huo haukufanikiwa alipoteza maisha wakati upasuaji ukiendelea na baadaye daktari mkuu aliyesimamia upasuaji huo pia alikutwa amepoteza maisha katika hali ya kutatanisha
licha ya watu wake wake wa karibu kueleza kuwa Amado ni mzima wa afya, Mamlaka za kiusalama zilitoa taarifa kuwa mharifu huyo amefariki dunia na kuacha mke na watoto watoto watatu ambao mmoja hao Julio Cesar aliuwawa kwa kupigwa risasi wiki iliyo[pita huko Mexico.
Mwisho.
No comments