Header Ads

Header ADS

Zuchu Azidi Kumfokea Nandy

 


SECOND lady wa lebo kubwa ya muziki barani Afrika ya Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othman ‘Zuchu’, anazidi kumfokea mwanadada mwenzake kunako anga la muziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfi nanga ‘Nandy’.

Zuchu ameweka rekodi ya kuwa msanii wa kike wa Afrika Mashariki mwenye wafuasi (subscribers) wengi zaidi kwenye Mtandao wa YouTube. Kabla ya Zuchu kujimwambafai, rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Nandy.

Kwa mujibu wa YouTube, kuna wakati Nandy huwa anapaa juu kumzidi Zuchu, lakini kwa kipindi kirefu sasa, Zuchu ameonekana kumhenyesha Nandy.

Zuchu amefanikiwa kuwa na wafuasi 547,000 akiwa amemuacha Nandy ambaye ana jumla ya wafuasi 546,000 kwenye mtandao huo (rekodi hizi ni hadi Jumamosi iliyopita).

Miongoni mwa nyimbo za Zuchu zinazotazamwa na kusikilizwa zaidi kwa wakati huu ni pamoja na Raha, Wana, Nisamehe, Hakuna Kulala, Cheche, Mauzauza, Litawachoma, Shangilia na nyinginezo.

Kwa upande wa Nandy, yeye anakimbiza na nyimbo zake kali zikiwemo, Na Nusu, Kiza Kinene, Acha Lizame na mpya inayokwenda kwa jina la Do Me akiwa ameshirikiana na Billnass.

Mpaka sasa, Zuchu ana jumla ya views (watazamaji) zaidi ya milioni 64.8 katika chaneli yake ya Mtandao wa YouTube ndani ya miezi michache tu huku akiwa ni mwanamuziki wa kike pekee ambaye anaongoza kwa kutazamwa na kufuatiliwa zaidi kwenye mtandao huo.

Zuchu amekuwa ni msanii ambaye ameweka rekodi nzuri kwenye muziki wake tangu alipotambuliswa kwenye muziki Aprili 8, mwaka huu.

STORI: KHADIJA BAKARI, DAR



No comments

Powered by Blogger.