Wema, Mobeto Walianzisha kumzima Zari
BAADA ya zilipendwa wao, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuteka mitandaoni na mitaani baada ya mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutua Bongo hivi karibuni, hatimaye zilipendwa wake wengine, Wema Isaac Sepetu na Hamisa Mobeto, wanadaiwa kuliamsha ili kuzima upepo huo.
Zaidi sana, ujio wa Zari unadaiwa kuwavuruga vilivyo mashabiki wa Wema na Mobeto.
Hali ya hewa ilianza kuchafuka mara tu baada ya mwigizaji Wema kusema hadharani kuwa, anamshangaa mwanamitindo Mobeto kujifanya mjuaji wakati alidumu na Diamond au Mondi kwa kipindi kifupi zaidi ukilinganisha na zilipendwa wengine wa jamaa huyo.
“Hamisa (Mobeto) alikuwa ananipenda mimi kama dada. Hata kipindi kile nikiwa na Nasibu (Mondi), Hamisa alikuwa ananipigia simu sana kutaka kuonana na mimi.
“Wewe unataka kuingia kwenye nyumba ya mwanaume, halafu unajifanya wewe ndiye wewe, unaleta ubosi, unasahau kwamba kuna mama na ndugu zake wengine ambao wametoka naye mbali
“Wewe ulikutana naye juzi tu kwa sababu mnapendana ndiyo unaanza kuleta ujuaji, lazima wakuchukie. Kwa hiyo ndiyo maana hiyo hali ilimkera Mama Dangote (Mama Mondi),” alisema Wema akielekeza tuhuma hizo kwa Mobeto kwamba alijifanya yeye ndiye yeye alipokuwa na Mondi kiasi cha kuwachukiza familia ya jamaa huyo.
Hata hivyo, madai yaliyopo kwa sasa ni kwamba, inasemekana kuwa mashabiki wa Wema na Mobeto wameamua kuikuza ishu hiyo ili kuzima kiki ya Zari kutua kwa Mondi ambayo ndiyo iliyokuwa imeteka mtandaoni.
Hata hivyo, kila mmoja; Wema na Mobeto wamekana kuwa na bifu na kwamba ni warafiki wakubwa, jambo linalothibitisha kwamba, walifanya hivyo kwa lengo la kuzima ujio wa Zari Bongo, jambo ambalo limeshindwa kufua dafu kwani bado mwanamama huyo ameendelea kutrendi mitandaoni.
Kwa muda mrefu, Wema na Mobeto walidaiwa kutopikika kwenye chungu kimoja hadi miezi kadhaa iliyopita walipotangaza kumaliza tofauti zao
No comments