Header Ads

Header ADS

Taifa Stars yabanwa mbavu, yachapwa 1-0



 TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imebanwa mbavu na kikosi cha Tunisia kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2022 nchini Cameroon.

Bao pekee la ushindi kwa Tunisia, kwenye mchezo wa kundi J uliochezwa Novemba 13 limefungwa na Youssel Msakni dakika ya 18 kwa mkwaju wa penalti.


Jitihada za Stras kupata bao zimekuwa ngumu usiku wa kuamkia leo nchini Tunisa kwa kubanwa mbavu mpaka dakika 90 kukamilika.


Nyota wawili wa Stars, Simon Msuva na Bakari Mwamnyeto walionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo huo ambao Tunisia waliutawala kwa kiasi kikubwa eneo la kiungo na ushambuliaji huku Aishi Manula akifanya kazi ya ziada kuokoa michomo minne ya hatari kipindi cha pili


Bakari Mwamnyeto, Erasto Nyoni na Shomari Kapombe mabeki wa Stars pamoja na Mohamed Hussein walikuwa na kazi ya kufanya kwa kuwa washambuliaji wa Sudan walikuwa wakiweka ngome lango la Manula.


John Bocco na Msuva walikuwa wakipata tabu mbele kwa kuwa ilikuwa ikiwalazimu kurudi nyuma kuokoa mashambulizi na kutengeneza nafasi za kwenda kufunga jambo ambalo limewafanya washindwe kufanya hatari kwa Tunisia.


Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Novemba 17, Uwanja wa Mkapa



No comments

Powered by Blogger.