Rais Magufuli "Utumbuaji Majipu Utaendelea"
Rais Dk. John Magufuli amesema utumbuaji wa majipu utaendelea katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Novemba 13, wakati akilihutubia bunge kwenye mkutano wa ufunguzi wa bunge la 12 jijini Dodoma.
"Kwa miaka mitano tumewafikisha mahakamani watumishi 32,535 kwa kashfa mbalimbali lakini watumishi wazembe bado wapo, wala rushwa bado wapo, mafisadi bado wapo, kwa kifupi niseme utumbuaji wa majipu utaendelea," amesema Rais Magufuli.
No comments