Rais Donald Trump apata pigo baada ya kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi kutupiliwa mbali
Rais Donald Trump amepata pigo baada ya kesi yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Marekani kutupiliwa mbali.
Hii ni baada ya timu ya kampeini ya Trump kuwasilisha kesi mahakamani iliyonuia kupinga matokeo ya kura zilizopigwa kwa njia ya posta katika jimbo la Pennsylvania.
Jaji wa mahakama ya jimbo la Pennsylvania, Mathew Brann, ametoa uamuzi kuwa timu ya kampeini ya Trump ilishindwa kutoa ushahidi wa kutosha kuonyesha udanganyifu ulifanyika katika uchaguzi wa Novemba 3, ambao Trump alishindwa na mpinzani wake Joe Biden wa chama cha Democrat.
Kesi hiyo iliyowasilishwa na wakili wa Trump, Rudy Giuliani, ilinuia kuzuia maafisa kuthibitisha ushindi wa Biden katika jimbo hilo, wakitoa sababu ya udanganyifu katika zoezi la kupiga kura kwa njia ya posta.
No comments