Mwanaume Aliyeanza Kupata Hedhi Kabla ya Kujigundua Ana Jinsia Mbili Asimulia
Katika umri wa miaka 22, niligundua kuwa mimi ni mtu mwenye jinsia mbili. Tangu wakati huo maisha yangu yamekua ya furaha kuliko awali ,”anasema Iryna Kuzemko.
Ni mmoja wa watu wengi ambao ”wana jinsia mpya” kote duniani kupitia upasuaji wenye utata walipokuwa bado watoto.
Intersex au jinsia mbili ni mwavuli unaotumiwa kujumuisha aina za utofati wa tabia 40 za jinsia ya kike na ya kiume .
Baadhi ni aina za homoni za mwili, nyingine hujitokeza katika muonekano wa mwili-kwa mfano watu wanaweza kuwa na mfumo wa viungo vya uzazi vya aina moja ya jinsia, na kuwa na muonekano wa sehemu za siri wa jinsia nyingine.
Watu wengi wenye jinsia mbili hupitia kipindi kigumu maishani mwao cha kutaka kupata majibu , mara nyingi baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupewa jinsia mpya .
Madaktari wanasema uamuzi wowote wa kuamua ni jinsia gani inayopaswa kuwa utambulisho wake moja haupaswi kuchukuliwa kama kitu cha kawaida -kipimo cha jeni au urithi cha kubaini jinsia ya mtoto na madaktari, wazazi, na wataalamu wa jeni hukubaliana kuangalia iwapo upasuaji huo unafaa kufanyika au la.
Lakini wanaharakati wa watu wenye jinsia mbili wanapinga kutokuwepo kwa dharura ya kuwapatia watoto wa aina hiyo utambulisho mpya wa kijinsia . Wanasema mtu hawezi kufanya uamuzi sahihi kuhusu jinsia yake katika utu uzima.
Wanaamini wazazi na madaktari hawapaswi kuwaamulia wao ni akina nani-mwanaume au mwanamke.
Wanawake wawili waliobadilishwa jinsia upya wanaelezea safari yao ya kujibubali :
Iryna Kuzemko, 27, mwanaharakati aliyezaliwa na jinsia mbili.
Iryna as a child
CHANZO CHA PICHA,IRYNA KUZEMKO
Maelezo ya picha,Iryna alikuwa bila kujua ana jinsia mbili
Nilikua kama msichana hadi nilipofika umri wa balehe. Watoto wa umri wangu walifikia kipindi cha balehe na sikupata hedhi.
Kwa muda mrefu nilibakia kuwa msichana tu ambaye hakuwa na matiti darasani.
Siku moja darasa letu lilipelekwa kutazama filamu kuhusu wasichana wanaobalehe.Ulikua ni uzoefu ulioniumiza sana.
Sikuelewsa ni kwanini kila mtu alikuwa anaelewa kadri filamu ilivyokuwa ikiendelea na mimi sikuelewa chochote.
Mama yangu na bibi yangu hawakuwa na hofu kwamba sikuwa ninakua kama wasichana wengine walisema: “Hakuna shida”. Kila kitu kitakuwa sawa kwa wakati sahihi. Lakini nilikuwa na umri wa miaka 14,
Niliwashawishi wanipeleke kwa daktari wa wanawake.
Daktari alisema ninahitaji kusasidiwa mayai ya uzazi yafanye kazi. Aliniandikia baadhi ya tiba ya “kuyapatia joto”.
Nilifanyiwa mara moja kwa wiki kwa miezi kadhaa, lakini hapakuwa na mabadiliko yoyote. Nilihisi hata kukanganyikiwa zaidi.
Nikiwa na umri wa miaka 15, baba yangu alinipeleka kwa madaktari mjini Moscow. Ninakumbuka jinsi walivyonipita haraka wakitembea. Hawakunielezea chochote -walimuita tu baba yangu ndani ya ofisi.
Iryna as an adult
CHANZO CHA PICHA,IRYNA KUZEMKO
Maelezo ya picha,Iryna
Baba yangu alisema ninapaswa kufanyiwa upasuaji mdogo, kama mara mbili. Sikujua nini walikuwa wananifanyia .
Wasichana shuleni kwetu waliniuliza, lakini hata mimi mwenyewe sikuelewa lolote.
Baadae nilimwambia baba yangu kuwa itakuwa bora kuondoa kila kitu kilichomo ndani yangu.
Na alijibu “Lakini kila kitu kiliondolewa!” Nilishituka . Hivyo ndivyo nilivyogundua kuwa mayai yangu yaliondolewa.
Kama mwanafunzi, niliingia katika kipindi cha kujichukia na kujikasirikia.
Nilipata video inayozungumzia watu wa jinsia mbili kwenye intaneti na kuona kwamba hadithi zao zinafanana na yangu.
Nilipata karatasi zote za matibabu na nikampigia simu daktari mjini Moscow, huku mama yangu akiwa amesimama kando yangu. Nilikuwa mwenye wasiwasi mkubwa.
Kwahiyo, nikiwa na umri wa miaka 22 niligundua kuwa miaka saba iliyopita, nilikuwa na manii (mfuko wa mbegu za kiume) na nyama za mwili ambazo haziwa zinafanya kazi zikiwa na nyama za mfuko wa mayai ya uzazi ambazo . Nimekuwa nikimeza tembe za homoni tangu wakati huo.
Niligundua kuwa nina homoni za urithi za kiume, pamoja na za kike. Nina mfuko wa uzazi.
Baada ya hayo, nilikuwa na mazungumzo makali na baba yangu.
Alisema kuwa wanasaikolojia wawili wa watoto walikuwa wamemshauri asiniambie kuhusu hilo.
Baba yangu hakukiri kosa lake: angepaswa kuniambia ukweli mara moja.Maisha yangu yangekuwa tofauti.
Sijawahi kuongea nae tena tangu wakati huo.
Siku chache baada ya taarifa hii , nilikuwa katika mkanganyiko na masikitiko makubwa . Sikujua jinsi ya kuishi tena. Lakini nilijikubali haraka.
Sasa nina neno la kueleza utambulisho wangu wa jinsia, Mwenye jinsia mbili “intersex” .
Kujiamini kwangu kumeongezeka kwa kiasi kikubwa .
Niliamua kuwa mtu wa bidii kuwasaidia watoto na walio katika umri wa balehe kuepuka kiwewe nilichopata.
Three intersex women
CHANZO CHA PICHA,IRYNA KUZEMKO, LIA AND OLGA OPINKO
Maelezo ya picha,Iryna Kuzemko, Lia na Olga Opinko wana jinsia mbili tofauti
Kauli ya daktari: Julia Sydorova, daktari wa watoto
” Ni nadra kwa madaktari hukumbana na tofauti za watu wenye jinsia mbili”
“Ni muhimu kutofautisha upasuaji wakati maisha ya mtoto yako hatarini, na kile kinachoitwa upasuaji wa kurekebisha mwili -cosmetic surgery.
Upasuaji huo hufanywa kwa watoto wachanga: Viungo vyao vya uzazi hutengenezwa na kuwa na muonekano wa kawaida.
Mtoto wa kike, kwa mfano, anaweza kuwa na sehemu zake za siri zenye muonekano wa kiume.
Anaweza kutengenezewa sehemu za kike, ili kumpa muonekano wa kile.
Ingawa hali hii haitishii maisha, kuna hofu ya kijamii. Mtoto wa aina hiyo anaweza kuangaliwa kwa kumshuku anapokuwa shuleni au anapokwenda kuogelea.
Upasuaji mara nyingi unaweza kuleta madhara kama vile kukosa hisia, kutokuwa na uwezo wa kuzaa, au maumivu ya kudumu.
Tiba ya homoni inaongeza hatari ya saratani. Ninapaswa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara, kwa mfano.
Ni muhimu pia kuelewa kuwa jinsia mbili haipaswi kukanganywa na aina ya jinsia ya mtu . Wengi wetu tuna jinsia tulizo nazo lakini kuna watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Watu wenye jinsia mbili wanafamilia na wanawatoto
Lia
CHANZO CHA PICHA,PICKPIK.COM
Lakini wakati huo huo, hadithi ya kila mtu ni ya kipekee: mchanganyiko wa muonekano unaweza kuonekana wakati mtoto anapozaliwa, lakini watu wengine wana muonekano wa kawaida, na utofauti wa jinsia kuonekana wakati wanapokuwa katika umri wa balehe.
Leo, wengi miongoni mwa wanafunzi wenzangu, waalimu na marafiki wananiunga mkono. Ninapata upendo mkubwa kutoka kwa watu wengi.
Tangu nilipoelewa na kujikubali, kila mwaka wa maisha yangu umekuwa wa furaha na furaha zaidi .
Hadithi yangu ilianza katika hospitali ya kujifungulia. Madaktari walimwambia mama yangu kwamba sehemu zangu za siri hazikuwa zimeumbwa zikakamilika , jambo linalozifanya kuonekana si za kike au za kiume.
“Mama, unahisi umejifungua mtoto kiume au wa kike?” walimuuliza mama yangu.
Mama yangu aliamua kunisajiri kama msichana. Hili lilikuwa ni kosa la kwanza walilofanya madaktari. Wasingemuachia wajibu wote mama.
Kwahiyo mwanzoni nilikuwa kama msichana na mama yangu alinipenda kama mtoto mwingine yeyote.
Kabla ya kwenda shule mama yangu alinipeleka kwa uchunguzi wa kimatibabu. Daktari katika kliniki ya watoto alimwambia mama yangu : “Kwani wewe ni mjinga? Una mvulana!”
Madaktari wengine walithibitisha kuwa nilikuwa mvulana na jina langu yakabadilishwa kwenye nyaraka zote.
Lia among some flowers
CHANZO CHA PICHA,LIA
Maelezo ya picha,Lia anasema mama alijihisi vibaya kwa maamuzi aliyofanya
Niliingia darasa la kwanza kama mvulana, lakini kulikuwa na watoto pale katika shule ya chekechea, ambao kila mmoja alinitambua kama msichana. Mama yangu alilazimika kunihamishia kwenye shule nyingine.
Tangu wakati huo, sikuwa na wasiwasi kuhusu kile kilichokuwa kinaendelea . Lakini nilipoona jinsi watu wazima walivyokuwa na wasiwasi , nikaanza pia kuhisi hofu na msongo wa mawazo.
Nilikataa kukata nywele zangu ndefu, lakini nikaanza kuvaa suruari na nguo ambazo kubwa kubwa. Ninaelewa kuwa waliniepusha na kuchagua jinsia yangu, jambo lililonifanya nitulie. Nimeshikilia mtizamo huu hadi leo.
Nilipokuwa na umri wa miaka 13 nilipata ajali, niligongwa na farasi . Niliamka nikijipata hospitalini nikiwa nimepata jeraha la uti wa mgongo.
Niliwekewa chuma kwenye mgongo wangu, kwa hiyo wauguzi wakaona sehemu zangu za sirina kunitania kwamba huwezi kujua mili ni mvulana au msichana. Hebu fikiria kuwa umepata ajali halafu unasikia haya.
Baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali, nililala nyumbani kwa mwaka mzima katika chumba ambamo niliwekewa kiti na bakuli mbili la chakula na la kujisaidia haja zote pamoja .
Mama yangu, bibi yangu na dada yangu walikuwa wakifanya kazi siku nzima na baba alituacha, kwa hiyo hapakuwa na mtu wa kuniangalia.
Madaktari hawakuamini kuwa nitaweza tena kutembea, lakini nilianza kufanya mazoezi na siku moja nikasimama bila usaidizi wa kifaa maalumu.
Shule palikuwa mahala pa kwanza nilipotaka kwenda-ilikuwa ni mwendo wa dakika 20, lakini baada ya ugonjwa ilinichukua saa mbili kufika huko.
Shuleni watoto walinizomea na kutupa mfuko wangu wa madaftari chooni. Walifahamu sikuweza kuwakimbiza.
Nilikuwa na umri wa miaka 16 nilipoamka na kuona damu kwenye kitanda change.
Nilipelekwa hospitalini na daktari akanifanyia uchunguzi .
Ghafla alipaza sauti : “Kuna mvuko wa uzazi hapa!” Alipuuza kabisa kwamba nilikuwa ninamsikia
Hivi ndivyo nilivyogundua kuwa nilikuwa na viungo vya kike vya siri – kwamba nilikuwa ni mvulana ambaye alikuwa amenza kupata hedhi.
Wakati ule, nilitaka waviondoe ndani ya mwili wangu, vile ambavyo sikuweza kuviona.
Hatahivyo, madaktari walitushawishi kuwa ilikuwa ni vyema kuacha viungo vyangu vya ndani, kwasababu vilikuwa vinafanya kazi kikamilifu, na vinaweza kuwa vya maana katika siku za usoni.
Kwahiyo nilifanyiwa upasuaji mara nne kwa miaka kadhaa na nikawa msichana.
Olga Onipko, miaka 35, mwanaharakati wa watu wenye jinsia mbili
Olga Opinko
CHANZO CHA PICHA,OLGA OPINKO
Wakati wote nimekuwa nikionekana kama msichana na nina mfumo wa kike pia.
Lakini nilipokuwa katika umri wa balehe,nilianza kuongezeka uzito wa mwili na nikawa ninakejeliwa.
Nilienda kufanya mzoezi mchana na usiku na kuchagua vyakula vya kula ili kupoteza uzito wa mwili lakini niliendelea kunenepa.
Nikiwa na umri wa miaka 24, nilifanya kipimo cha homoni, ambacho kilibaini kuwa mfumowangu ulikuwa umevurugika kabisa, lakini sikuwa na nilikuwa mtu mwenye jinsia mchanganyiko.
Niliambiwa kuwa vipimo vilionesha kuwa kiwango cha homoni kilikuwa kimepita uwiano unaotakikana lakini baada ya muda nilipata ndevu na shingoni.
Fikiria nilivyojihisi kama msichana mwenye umri wa miaka 25 ambaye anataka kutoka kuhudhuria sherehe na kupata marafiki.
Niliacha kumeza hizo tembe za homoni, lakini kuanzia wakati huo, nilipokuwa na pesa na nguvu,niliwatembelea madaktari zaidi.
Daktari mmoja alijitolea kufanya uchunguzi wa mpangilio jeni zangu.
Nashukuru uchunguzi huo, kwani uliniwezesha kufahamu kuwa ninahomoni za kiume, ikimaanisha kuwa mimi ni mtu wa jinsia mbili.
Awali nikiwa na umri wa miaka 24, niligundua kuwa nilikua msagaji.
Kwahiyo jiulize hisia nilizonazo: Ujana wangu wote nilikuwa na wasi wasi kuwa sikuwa mwembamba vya kutosha, halafu nikabaini kuwa nilikuwa mpenzi wa jinsia moja na sasa nilikuwa ninajiuliza iwapo mimi ni mwanamke aliyekamilika . Mimi ni nani hasa?
Kaka yangu alitaka kujua kuwa mtu mwenye jinsia mbili ni mtu wa aina gani.
Aaah, hiyo ni poa. Dada zangu wakubwa walikuwa na hofu zaidi. Wazazi wangu walinikubali,wananipenda, lakini hawawezi kuzungumzia hali yangu.
Ni vigumu pia kwao kukubali kuwa mpenzi wangu ni mtu wa kawaida .
Alizaliwa kama msichana lakini hajioni kama mmoja wa jinsia moja kati ya hizo.
Kwangu mimi mtu wa jinsia mbili anahitaji kusikilizwa.
Wanasema upasuaji waliofanyiwa wakiwa watoto uliwaathiri, kwamba wanahisi tofauti na kile ambacho daktari aliwaamulia
Madaktari na wazazi wanajaribu kumbana mtoto mwenye mchanganyiko wa tabia za jinsia katika muundo wa tabia za “kike au za kiume”.
Jamii inahisi haja ya kuwafanya watu hawa “wakubalike”.
Watu wa aina hii wanadhalilishwa na wale wenye hofu kubwa ya kuwa na mtu asiye wa kawaida na ambaye hakutarajiwa.
Lakini labda ukweli ni kwamba watu wa aina hii wanaweza kuzaliwa.
Maumbile wakati mwingine hayajitokezi katika hali ya jinsia inayofanana na jinsia za kike au za kiume.
Profesa wa akili na viungo vya mwili -Serhiy Kyryliuk anasema ana wagonjwa wa aina hiyo
Wakati watu wenye jinsia mbili wanapotambua kuhusu upasuaji waliofanyiwa walipokuwa watoto wanahisi hasira sana.
Suala kuu sio kuacha hasira hii iingie moyoni. Unapaswa kuishi.
Watu wenye jinsia mbili wanapojikubali wenyewe na kutambua upekee wao, wanakua wazuri.
Sura zao zinaanza kung’ara . “
No comments