Mhudumu wa afya wa Israeli afutwa kazi baada ya kutemea mate picha za Yesu
Mhudumu wa gari la kubebea wagonjwa aliyenaswa na kamera nchini Israeli ,alizitemea mate picha za Yesu alipotembelea nyumba za wakristo kuwafanyia kufanya vipimo vya corona amefutwa kazi.
Daktari huyo alionekana akiondoa usoni barakoa na mavazi mengine ya kujikinga na kuzitemea mate picha tatu zilizokuwa kwenye makazi hayo ya magorofa katika eneo la Jaffa mjini Tel Aviv.
Alipoulizwa , daktari huyo alidai kuwa picha za aina hiyo ni aina ya sanamu zinazozuiwa na Biblia ya Kiyahudi.
Mamlaka ya huduma za magari ya wagonjwa nchini Israeli imesema "inalaani vikali " kitendo chake.
Bw David Adom ambaye ni mfanyakazi wa huduma hiyo (MDA) amesema kuwa ulikuwa ni "uwakilishi usio na thamani wa shirika " na akafutwa kazi mara moja.
Tukio hilo lilitokea Jumapili wakati alipokuwa ameenda kwenye jengo -ambalo wakazi wake wote ni Wakristo, kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari.
Picha za kamera za usalama zilimuonesha akiondoa barakoa yake, na magwanda mengine ya kujikinga corona na kuzitemea picha tatu picha hizo moja baada ya nyingine.
Anaonekana akuvaa tena barakoa yake na kuingia kwenye lifti baada ya kitendo hicho.
Alipokuwa akiondoka kwenye jengo hilo, alikabiliwa na wakazi ambao walirekodi video ya malumbano hayo kwenye simu zao za mkononi.
Wakati wakazi walipomuuliza ni kwanini anatemea picha za Yesu, alijibu : "Katika dini ya juda hii ni ibada ya kigeni ."
Video inaonesha wakazi wakimuambia mhudumu huyo wa afya: "Ulitemea picha yangu, ambayo ninaiamini, mbele ya macho yangu, mbele macho yangu. Kwanini ulifanya hivyo?"
Mhudumu huyo alijibu: "Katika Torah yetu imeandikwa kwamba ni ibada ya kigeni kwa hiyo inapaswa kuepukwa iwezekanavyo ," kabla ya kulalamika kwa wakazi kwamba hakuwa amevaa barakoa.
Tukio liliripotiwa kwa mamlaka ya huduma za magari ya kubebea wagonjwa -MDA, ambao walimuhoji maswali na kumfukuza kazi.
Katika ujumbe wa Twitter, mamlaka ya huduma za ilisema "inalaani vikali " kile kilichotokea, na kuongeza kuwa imewaajiri wafanyakazi kutoka dini na jamii mbalimbali.
No comments