Libya na Tunisia zafungua mipaka iliyofungwa kutokana na Covid-19
Mipaka ya Ras Jadir na Wazin Zahiba inayounganisha Libya na Tunusia imefunguliwa tena upya baada ya kufungwa kwa kipindi cha miezi 8 kutokana na janga la corona (Covid-19).
Wizard ya Mambo ya Nje ya Libya ilituma barua rasmi kwa Wizara ya Mambo ya Ndani tarehe 11 Novemba, na kuitaka mipaka ya inayounganisha Libya na Tunisia ifunguliwe kuanzia siku ya Jumamosi tarehe 14 Novemba kufuatia makubaliano ya kiafya kuhusu janga la Covid-19 kutiwa saini.
Wizara ya Uchukuzi ya Tunisia ilitoa maelezo hapo jana na kutangaza mpango wa kuanzisha tena upya safari za ndege za kuelekea Libya siku ya Jumapili tarehe 15 Novemba zilizokuwa zimesitishwa kwa miezi 8 kama mojawapo ya hatua za kukabiliana na janga la Covid-19.
No comments