Jack Wolper "Mwanaume Atakayeweza Kunipa Mimba Nitamjengea Nyumba ya Kifahari"
Nyota wa sinema Bongo, Jackline Wolper ameibuka na kutoa neno la kifamilia kwamba, mwanaume atakayeweza kumpa kibendi, yeye atamkirimia kwa kumjengea nyumba ya kisasa yenye mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Wolper ambaye kiasili ni Mchaga, ameyasema hayo jana alipokutana laivu na mwandishi wa habari hii, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa, amekuwa akipata maneno na matamko kutoka kwa watu mbalimbali kwamba, azae sasa, hata mtoto wa kiume.
'Kila nikikatiza maneno ni hayohayo. Sasa mimi nasema, kidume atakayejitokeza akaweza kunipa ujauzito nitamjengea nyumba ya kisasa.
"Nyumba ya vyumba vitatu. Kimoja selfu. Sebule kubwa, toilet ya jumuiya, stoo, bafu na choo ikiwa imezungukwa na ukuta wa ulinzi," alisema Wolper ambaye ukoo wake ni wa Masawe.
Alipoulizwa huyo mwanaume atampataje yeye, alijibu: "Mwenye uhakika anikabili. Mimi nipo." Kuhusu sifa ya mwanaume anayemtaka ampe ujauzito, Wolper alisema 'anayeweza kunipa mimba. Ndiyo sifa namba wani."
Hivi karibuni, mastaa wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel Grayson 'Jujuman' na Rose Donatus Ndauka wamejifungua. Wote ni watoto wao wa pili kwenye uzao.
Bado jamii inawatupia macho mastaa hawa wawili, Wema Sepetu, Wolper Kuleta familia zap kwani hata Gigymoney ana mtoto.
Hata Hivyo, mara kadhaa, Wolper amewahi kunukuliwa akidai ni mjamzito. Haijajulikana kama huwa zinatoka au anateleza ulimi. Mungu ndiyo anajua.
No comments