Harmonize: Tunaua lugha yetu nzuri ya Kiswahili, tunataja sana viungo vya pilau kwenye ngoma zetu
Kupitia ukurasa wake wa Instagram upande wa Insta story, Harmonize aliandika kwamba “Napenda jinsi ma-dj’s wa Tanzania kutocheza sana muziki wa Bongo Club, tunataja sana viungo vya pilau kwenye ngoma zetu, tunatakiwa kubadilika tunawapa shida waache kupiga nyimbo kama mazerati, no stress, woman au mapiano sound halafu wakapige pembe la ng’ombe ukiuliza ni uzalendo, hivyo tutakuwa hatutangazi bali tunaua lugha yetu nzuri ya Kiswahili kwa sauti mbaya tunazozitumia” ameeleza Harmonize
Aidha ameongeza kueleza kuwa “Nawaamini ma-producer wa Tanzania kwa asilimia 100, kipaji ni msanii kufanya uamuzi na kutengeneza njia za huu muziki kuwa burudani ya kweli, tunahitaji kubadilika tunaweza kukimbiza dunia”
No comments