Header Ads

Header ADS

Georgia Yarudia Kuhesabu Kura, Biden Amgaragaza Trump Tena



RAIS Mteule wa Marekani, Joe Biden (78),  ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa Jimbo la Georgia baada ya zoezi la kurudiA kuhesabu kura kwa mkono kukamilika.


Ushindi wake unafanya hii kuwa mara ya kwanza tangu mwaka 1992 kwa Chama cha Democratic kushinda Jimbo hilo ambalo limekuwa upande wa Republican kwa muda mrefu.


 


Hadi sasa, Biden ana jumla ya kura 306 za Wajumbe wa Uchaguzi huku mpinzani wake, Rais Donald Trump akiwa na 232.


 



No comments

Powered by Blogger.