Dkt. Tulia Ashinda Unaibu Spika
Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Tulia Ackson amechaguliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la 12 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2020-2025) baada leo Alhamisi, Novemba 12, 2020 Bungeni jijini Dodoma.
Dkt. Tulia ambaye alikuwa mgombea pekee wa Unaibu Spika, amepitishwa na bunge hilo baada kushinda kwa kupata kura za NDIYO 350 kati ya kura 354 zilizopigwa huku kura 4 zikiwa za HAPANA ambapo tayari Spika Job Ndugai amemuapisha Dkt. Tulia kuanza majukumu yake.
Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Dkt. Tulia amesema; “Asanteni sana kwa kura nyingi mlizonipa, wote tungeweza kuwa kwenye nafasi hii ambayo mimi mmeniheshimu siyo kwamba mimi ni bora lakini ni wazi mimi mmenitanguliza mbele yenu na nitajitahidi kuwa wa mfano huko mbele mlikonitanguliza.”
No comments