Header Ads

Header ADS

Bernard Morrison, Chama Watumiwa Ujumbe na Wagosi wa Kaya

 


BEKI tegemeo ndani ya kikosi cha Coastal Union, Hance Masoud, amesema kuwa hawana hofu na mchezo wao wa leo dhidi ya Simba Uwanja wa Sheikh Amri Abeid watapambana kupata pointi tatu muhimu.

Masoud ameweka wazi kuwa hawana presha na safu ya viungo wa Simba inayoongozwa na Clatous Chama mwenye mabao mawili na pasi tano za mabao pamoja na Bernard Morrison mwenye pasi moja bao kati ya mabao 22 yaliyofungwa na Simba.


Akizungumza na Saleh Jembe, Masoud amesema kuwa wamepewa mbinu zitakazowazuia wapinzani wao na watazifuata ili wapate pointi tatu kwenye mchezo wao.


“Tumejiandaa kushindana ndani ya uwanja nje ya uwanja wao acha wapambane wanavyojua.Hatuwaogopi ila tunawaheshimu, ukiwazungumzia akina Chama,(Clatous), Morrison,(Bernard) wote ni wachezaji na sisi hatuchezi na majina tunacheza na timu itakayokuja uwanjani.


“Morali ni kubwa tupo vizuri na tunahitaji pointi tatu kama ambavyo wao wanahitaji kwa nafasi ambayo tupo lazima tupambane ili kuzidi kuwa imara zaidi, mashabiki wajitokeze kutupa sapoti,” amesema Masoud.


Chini ya Juma Mgunda ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi 10, Masoud mechi zote ambazo ni sawa na dakika 900 alianza kikosi cha kwanza,inakutana na Simba iliyo na pointi 20.



No comments

Powered by Blogger.