Header Ads

Header ADS

Alici Akeys amwagia sifa Diamond Platnumz



Mshindi wa tuzo za Grammy mara 15, Alici Akeys, amemsifu msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz, kwa aina yake ya uimbaji ambayo ameiita ya kipekee.

Alicia ameyasema hayo alipokuwa akifanya tathmini ya album yake aliyoitoa siku za karibuni ambapo Diamond ameshiriki kwenye wimbo uitwao ‘Wasted Energy.’


“Nimependa Diamond kuwa sehemu yaa album yangu, msanii wa Tanzania mkali ambaye ameibariki album yangu kwa aina yake ya uimbaji ya kipekee,” alisema Alicia Keys.


Diamond Platnumz ameweka historia ya kuwa Muafrika wa kwanza kushiriki kwenye Album ya msanii wa Marekani.



No comments

Powered by Blogger.