Header Ads

Header ADS

Afariki Dunia Baada ya Kugongwa na Treni, Kamanda Simiyu Afunguka

 


Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Galula Luhende (50), mkazi wa Malampaka, wilaya ya Maswa, mkoa wa Simiyu, amefariki dunia baada ya kugongwa na Treni usiku wa kuamkia leo Novemba 20, 2020.

Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, ACP Richard Abwao, amesema kuwa treni hiyo ilikuwa ikitokea Jijini Mwanza kwenda DSM na kwamba kabla ya ajali ilisimama Malampaka kupakia abiria.


“Marehemu alikuwa akidandia Treni hiyo iliyokuwa imeanza kuondoka, ndipo alipoteleza na kuanguka na kukanyagwa miguu” ACP Abwao.


“Marehemu huyo kabla ya kufariki, alikimbizwa Kituo cha Afya Malampaka na baadaye kuhamishiwa Hospitali ya wilaya ya Maswa kwa matibabu” ACP Abwao



No comments

Powered by Blogger.