ACT-Wazalendo wadai wanachama wao waliotoweka wameanza kupatikana
Unguja. Chama cha ACT-Wazalendo, kimesema wanachama wao 18 wanaodaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana, wameanza kuachiliwa huru kwa staili ya kutupwa katika maeneo mbalimbali mjini Unguja.
Mbali na hilo, kimeitaka Serikali kuwaachia huru au kumfikisha mahakamani Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Nassor Ahmed Mazrui na mwenzake wanaoshikiliwa na polisi kwa zaidi wiki mbili baada ya kukamatwa Oktoba 28 mjini Unguja.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu katibu wa haki za binadamu na makundi maalumu wa ACT-Wazalendo, Pavu Juma Abdallah wakati akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya ofisi za chama hicho Vuga, Unguja.
Katika maelezo yake, Pavu alidai wanachama hao waliochukuliwa kwa nyakati tofauti kuanzia mwisho wa mwezi uliopita, walianza kupatikana juzi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Unguja wakiwa wametupwa huku wengi hali zao zikiwa mbaya kutokana na majeraha.
“Baadhi yao hali zao nzuri, lakini wale waliokuwa na hali mbaya tumewapeleka hospitali kwa ajili ya matibabu. Wanachama hawa walitupwa maeneo ya Kidele, Makunduchi na Kitope,”
“Juzi (Alhamisi wiki hii) saa 10 jioni ndiyo walianza kutupwa kwenye mapori na barabarani. Uzuri wenyewe wanafahamika ndiyo maana ilikuwa rahisi kupata msaada na wapita njia,” alisema Pavu.
Pia Soma
Gumzo Biden naye kuwa na asili ya India
Gumzo Biden naye kuwa na asili ya India
Moto uliowashwa na mama waua mtoto
Moto uliowashwa na mama waua mtoto
Wapinzani watoa ya moyoni hotuba ya Rais Magufuli bungeni
Wapinzani watoa ya moyoni hotuba ya Rais Magufuli bungeni
Wakazi Dar waeleza sababu kujitokea upimaji bure wa afya
Wakazi Dar waeleza sababu kujitokea upimaji bure wa afya
ADVERTISEMENT
Katika mkutano huo, Pavu aliwataja waliookotwa kuwa ni Suleiman Ahmed Suleiman mkazi wa Mahonda, Ashraff Hafidh Juma, Mwinyi Mohamed Said, Seif Haroub Amour, Mohamed Soud na Ameir Ameir Soud wote wanaishi eneo la Kinduni.
Wengine ni Mohammed Said Amour (Raha leo), Khamis Hassan Vuai na Ali Naimu Ali (Makunduchi), Nahoda Khamis Haji, Ali Mati Wadi, Mcha Hassan Ajem, Ziadi Makame Salum, Foum Shombe Kombo, Ambali Ali Mcha (Matemwe) na Hassan Haji Fatawe (Paje).
“...hatutalinyamazia suala hili, tutawaambia Wazanzibari wenzetu na Watanzania wenzetu na jumuiya za kimataifa. Tunataka tume ya uchunguzi kuchunguza matukio yote ya ukiukwaji wa haki za binadamu.”
“Polisi ichukue hatua za kisheria kwa watu wote waliohusika kuwachukua wanachama hawa kisha kuwatupa katika maeneo mbalimbali,” alisema Pavu.
Kuhusu Mazrui na Ayoub Bakar waliokamatwa na polisi tangu Oktoba 28 Mjini Unguja wakidaiwa kukutwa na vifaa vya kuingilia mfumo wa uchaguzi mkuu, mwanasheria wa chama hicho, Omar Said Shabaan alisema walipeleka ombi la kuitaka mahakamani kuu ya Zanzibar kutoa amri kwa polisi kuwaachia au kuwapeleka mahakamani kwa makosa wanayotuhumiwa.
Kwa mujibu wa Shaban, waliitaka mahakama kuwaita kamishna wa polisi wa Zanzibar na naibu mkurugenzi wa makosa ya jinai kufika mbele ya mahakama jana kueleza kuhusu kushikiliwa kwa Mazrui na mwenzake bila kufikishwa katika chombo hicho cha kutoa
“Licha wito huo wa mahakama hawakuweza kutokea, badala yake walitokea wanasheria wao wa polisi na wale wa Serikali na wameeleza sababu za kujibu viapo lakini waliomba kupewa muda wa kujibu kwa maandishi. Baada ya majadiliano ya pande mbili mahakama imetoa amri wajibu viapo Novemba 17 na ombi litasikilizwa Novemba 18 kisha kutolewa uamuzi,” alieleza Shabaan.
No comments