Zuchu Anabebwa au Jitihada Zake?
KATIKA orodha ya wasanii wa kike wanaopepea kwenye gemu la Bongo Fleva, itakuwa ni ngumu kuacha kulitaja jina la Zuchu, msanii chipukizi aliyepokelewa vizuri na mashabiki.
Zuchu ni memba mpya wa lebo kubwa inayomilikiwa na mwanamuziki mkubwa hapa Bongo na Afrika Mashariki, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ama Mondi, ya Wasafi Classic Baby (WCB). Jina lake halisi ni Zuhura Othman ambapo mashabiki wanamtambua kama Zuchu.
Ni mtoto anayetokea kwenye familia ya vipaji, kwani mama yake mzazi ni mkongwe na malkia wa mipasho hapa Bongo, Bi. Khadija Omari Kopa.
Zuchu alisainiwa rasmi miezi mitano iliyopita kama msanii kwenye lebo hiyo na kuongeza idadi ya wasanii wa kike kwenye lebo hiyo, ambapo nafasi ya u-first lady inashikiliwa na mwanamuziki na dada wa Mondi, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’.
Tangu kusainiwa kama memba wa lebo hiyo, Zuchu amekuwa akifanya maajabu kila kukicha, kwani mpaka sasa anakimbiza vilivyo kila kona ambayo kazi zake zipo.
Amekuwa akisifi ka kuwa kama msanii mwenye kipaji katika utunzi na hata uimbaji wake, ukiachilia mbali uvumilivu wake katika kuitafuta nafasi ya kuwa msanii wa lebo ya Wasafi.
Katika historia yake ya muziki mpaka kufi ka Wasafi , Zuchu alihaso sana mpaka kuipata nafasi ambayo yupo sasa. Alikaa miaka takriban minne bila kupata nafasi ya kuachia ngoma na ikafanya poa kama ilivyo sasa.
Zaidi ya yote, alikuwa ni msanii maalum kwa ajili ya kufanya jingo za Wasafi Media, huku akiibia kama msanii wa kuingiza back vocal kwenye baadhi ya ngoma, na hiyo ni kwa msaada wa Abdul Idd ‘Lava Lava’ ambaye ni memba mwingine wa lebo hiyo.
Zuchu alipita kwenye msoto huo bila kujua kuwa kuna jambo ambalo Mwenyezi Mungu alikuwa akimuandalia jambo ambalo lingefuta machungu ya miaka aliyohaso kuipata nafasi, japo ya kufanya kazi na mwanamuziki mkubwa kama Mondi.
Makala haya yanakudadavulia mafanikio ambayo kwa sasa yamekuwa ni kama mwanga kwa Zuchu na kumfanya aonekane msanii anayepasua anga. Mafanikio yake mara nyingi yamekuwa yakijadiliwa kwa namna mbili; kusaidiwa na uongozi unaomsimamia wa WCB, kwani ni uongozi mkubwa na wenye uwezo wa hali ya juu hata kwa upande wa koneksheni. Pia, jitihada zake mwenyewe, kwani amekuwa na uvumilivu, pia kajaaliwa vipaji ndani yake.
NGOMA ZAKE ZILIVYOTIKISA
Baada ya kusajiliwa na lebo hiyo, Zuchu alifanikiwa kutoa ngoma zake ambazo zilifanya vizuri, huku akitambulika na ngoma ya Wana na ambayo ilifanya vizuri, na mpaka sasa ina watazamaji takribani milioni sita ndani ya muda wa miezi 4.
Baada ya ngoma hiyo, Zuchu akaendelea kuachia mikwaju mikali, ambayo nayo ilifanya poa kwenye platform zote ikiwemo mtandao wa YouTube. Ngoma kama Kwaru, Nisamehe, Raha, Mauzauza, Hakuna Kulala, Ashua na Tanzania ya sasa zimefanya poa, kwani mpaka sasa zimejikusanyia watazamaji takribani milioni 33 kwa muda wa miezi mitano ya gemu la muziki wake.
MKWANJA MREFU ANAOINGIZA
Kupitia ngoma zake jinsi zinavyofanya poa kwenye mitandao ya kupakua muziki na kazi za wasanii, Zuchu anaingiza mkwanja mrefu kwa kila mwezi. Inakadiriwa kuingiza kiasi cha zaidi ya dola 1900 mpaka 29,000 kwa mwezi, ambayo ni sawa na shilingi milioni 66.1, kiwango ambacho anawafunika wasanii wengi tu ambao wamemtangulia kwenye zake? na ambayo ilifanya vizuri, na Nisamehe, Raha, Mauzauza, Tanzania ya sasa zimefanya gemu.
SHOO KALI
Julai 18 mwaka huu, Zuchu aliangusha bonge moja la shoo pale Mlimani City, I AM ZUCHU Asante Nashukuru, shoo ambayo ilikuwa ni habari ya mjini, kwani alijaza nyomi la watu tena kwa kulipia kiingilio chenye hadhi.
Katika shoo hiyo, Zuchu aliwaonesha Watanzania ni jinsi gani alivyo na kipaji na si longo longo. Jambo ambalo liliweka historia katika shoo hiyo, ni baada ya Zuchu kupanda jukwaa moja na kupafomu na mwanamuziki mkubwa mkongwe na malkia wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’ ama Jide.
Zuchu na Jide walipafomu ngoma ya pamoja na mpaka hapo, Zuchu akafanikiwa kutengeneza ukaribu mzuri na mkongwe huyo wa muziki.
Baada ya shoo hiyo, Zuchu aliwahi kufanya poa tena kwenye tamasha ambalo liliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pale viwanja vya Uhuru, kiasi cha kufanya mashabiki kumpigia saluti mwanadada huyo.
HESHIMA MITANDAONI
Jambo lingine kubwa ambalo Zuchu amelipata, ni kupata tuzo ya kufi kisha subcribers zaidi ya laki moja kwenye mtandao wa YouTube.
KUKUBALIKA KWA VIONGOZI
Rekodi nyingine ambayo Zuchu ameweza kuivunja, ni kukubalika kwa viongozi akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli. Tukio hilo lilitokea kwenye mkutano mkuu uliofanyika mjini Dodoma, ambako walipanda wasanii kibao jukwaani akiwemo Zuchu na rais, kuonesha kukubali kazi za Zuchu.
Kwa mafanikio haya, unaweza kusema Zuchu kabebwa na lebo, kwani ni lebo kubwa inayojulikana au lakini pia jitihada zake zimechangia. Ushauri wa bure, Zuchu asibweteke kwa haya anayoyapata, zaidi ni kuongeza juhudi.
No comments