Header Ads

Header ADS

Zari Yamfika Mazito Kutoka Kwa Wananzengo




Mwanamama mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa muziki barani afrika, Nasibu abdul ‘Diamond Platnumz’ yamemfika mazito kutoka kwa wananzengo, kisa kikiwa ni mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto.

Chanzo cha yote ni baada ya Mobeto kumposti Diamond au Mondi ambaye naye pia ni mzazi mwenzake kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Zari amejikuta akishambuliwa kutokana na kile alichokiposti Mobeto kuhusu Mondi kuwepo nyumbani kwake huku akiwa na mtoto wao, Abdul Nasibu ‘Dyllan’

Mobeto aliposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonesha baba na mwana wakiwa na furaha kwelikweli.Baada ya kuposti video hiyo, mashabiki waliibuka na kuanza kumshambulia Zari kuwa watu na baba zao yeye yuko wapi?“Watu na baba zao, wale Wasauzi (Zari na wanaye Tiffah na Nillan) wako wapi, mbona Simba (Mondi) haendi huko?’’ Aliandika shabiki mmoja.

Hata hivyo, baadhi ya maoni hayaandikiki kwa kuwa yanamuondolea Zari utu, lakini wapo walioonesha kumtetea mwanamama huyo kwa kusema Mobeto alifanya makusudi ili kuwaumiza ‘wake wenzake’ ambao wamezaa na Mondi.

“Kuna wanawake wana makusudi jamani, sasa huyu Hamisa (Mobeto) kumposti baba Dyllan mitandaoni ni makusudi tu, maskini Zari, katulia kimya hata hajibu,’’ aliandika mdau mwingine.


Mbali na Zari kushambuliwa kwa posti hizo kiasi cha kuonekana kuwa yale mahaba yake aliyokuja nayo kwa kasi mpaka kufikia kununuliwa gari kwa sasa yameisha, Mobeto ndiyo kwanza anaonekana ameanza vibweka vyake.Zari na Mondi wamejaaliwa watoto wawili ambao ni Tiffa na Nillan, kabla ya kuachana kwao miaka mitatu iliyopita sababu ikiwa ni Mobeto kuchepuka na jamaa huyo kiasi cha kumbebea hadi mimba





No comments

Powered by Blogger.