Samsung na LG Wasitisha Kuwauzia Huwawei Vioo va Simu
Kampuni za Vifaa vya Kielectroniki za Samsung na LG zimesitisha rasmi mkataba wa kuiuzia kampuni ya Huawei vioo au ‘screen panels’ zinazotumika kwenye simu.
Kampuni ya Samsung ndiyo muuzaji mkubwa wa vioo vya simu ama display za OLED, AMOLED na LCD zinazotumika kwenye simu nyingi Duniani. Wamesema wanasitisha mkataba ili kuendana na matakwa ya Marekani na kuepuka kukabiliana na vikwazo vya Marekani.
Marekani imetishia kwamba Kampuni yoyote Duniani itakayoiuzia vifaa Kampuni ya Huawei bila kibali chake itakabiliwa na vikwazo vya kiuchumi. Hii ni kutokana na mzozo wa Kidiplomasia unaoendelea kati ya Marekani na China.
No comments