Saed Kubenea apandishwa kizimbani, Akosa dhamana na Kurudishwa rumande
Mbunge wa Jimbo la Ubungo aliyemaliza muda wake Saed Kubenea amepandishwa kizimbani mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Arusha akituhumiwa kwa makosa mawili likiwemo la kutatisha fedha na kuziingiza nchini bila kibali.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Martha Mahumbuga jopo la mawakili wanne wa serikali wameeleza kuwa mnamo tarehe tano mwezi wa tisa huko Namanga mpakani mwa Tanzania na Kenya mtuhumiwa alikutwa na dola za Kimarekani 8000 hela za Kenya 491,700 na fedha za Kitanzania 71,000.
Mtuhumiwa huyo anatuhumiwa kukiuka sheria za kuvuka mpaka kwenda nchi jirani ya Kenya na kurejea nchini Tanzania kwa kutumia njia zisizo rasmi.
Kutokana na kosa la kutakatisha fedha kutokuwa na dhamana mtuhumiwa amepelekwa gerezani hadi tarehe 21/09/2020 kesi hiyo itakapotajwa.
No comments