Mhadhiri wa chuo kikuu Marekani aliyedanganya kuwa ni Mmarekani mweusi ajiuzulu, aeleza sababu
Mhadhiri wa chuo kikuu nchini Marekani ambaye anachunguzwa baada ya kukiri kwamba alidanganya yeye ni mweusi amejiuzulu , Chuo kikuu cha George Washington kimethibitisha.
Jessica Krug, profesa mshiriki wa Chuo Kikuu cha George Washington, alikiri kwamba yeye ni ”mzungu mwenye asili ya kiyahudi” na mwanamke kutoka mji wa Kansas.
Ujumbe huo ulisema: “Nimejijengea maisha ya uongo kwamba mimi ni mtu mweusi, na kudanganya katika kila hatua ya maisha yangu,”
Kulingana na makala iliyochapishwa Alhamisi, Jessica Krug alisema aliamini visivyo kuhusu utambulisho, ” kwamba sikuwa na haki ya kudai: Ni mwafrika wa kwanza kutoka Afrika Kaskazini, ni mtu mweusi mwenye asili ya Marekani, kisha mwenye asili ya Carribean kutoka Bronx”.
No comments