Mghana Wa Yanga Afichua Siri Ya Staili Yake Ya Kushangilia
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mghana, Michael Sarpong amefichua siri ya kwa nini akifunga bao anashika macho kufuatia kufanya hivyo katika mechi mbili alizofunga tangu ajiunge na timu hiyo.
Mshambuliaji huyo amejiunga na Yanga akitokea Rayon Sport ya nchini Rwanda ambapo alifanikiwa kufunga mabao 30 katika msimu miwili aliyoweza kucheza kabla ya kujiunga na Yanga ambapo hadi sasa tayari amefunga mabao mawili katika mechi mbili alizocheza.Sarpong amefunguka kuwa amekuwa akishangilia kwa kuonyesha ishara ya kushika macho akiamini kila anapofunga inatokana na uwezo wa Mungu na siyo matendo yake.
“Nashukuru napata nafasi ya kufunga kwangu ni jambo kubwa lakini hii inatokana na ushirikiano wa timu nzima ambayo tumekuwa tukipambana, matokeo hayakuwa mazuri katika mechi yetu ya kwanza lakini bado hatujapotea.“Unajua kushangilia kule huwa namaanisha kwamba kufunga kwangu mabao siyo uwezo wangu bali ni Mungu ndiyo anasababisha nafunga wala hakuna jambo lingine zaidi ya hilo,” alisema Sarpong.
No comments