Mbadala wa Samatta atua Aston Villa, hofu yatanda Mtanzania huyo kutimka PL
Klabu ya Aston Villa imekamilisha usajili mshambuliaji, Ollie Watkins akitokea katika timu ya Brentford kwa kandarasi ya miaka mitano.
Usajili wa striker huyo umevunja rekodi ndani ya klabu ya Aston Villa kwa dau la paundi milioni 28 ambayo inaweza kufikia hadi milioni 33 huku akipewa nafasi kubwa ya kuja kuchukua nafasi ya ushambuliaji.
Kutokana na ukubwa wa pesa iliyotumika kwa dau lililoweka rekodi katika usajili wa mshambuliaji huyu, Ollie Watkins kunamfanya wadau wa soka kuamini kuwa Samatta anatakiwa ajipange upya ili kuipigania nafasi hiyo hasa kutokana na Mbwana kufunga magoli mawili pekee ndani ya miezi nane aliyokuwepo Aston Villa.
Kocha wa Aston Villa, Dean Smith amesema kuwa mchezaji huyo alikuwa chaguo lake namba moja katika dirisha hili la usajili ”Alikuwa kipaumbele changu namba moja na nafurahi sana kumpata. Tunatarajia atatuonyesha ubora aliyokuwanao.”
Mbwana Samatta amesajiliwa na Aston Villa katika dirisha la mwezi Januari kwa daua la paundi milioni 8.5 lakini sasa anahusishwa kutimkia katika klabu ya Besiktas ya nchini Uturuki.
Watkins mwenye umri wa miaka 24 amefunga jumla ya mabao 26 msimu uliyopita wa 2019/20 katika ligi ya Champions League
No comments