Header Ads

Header ADS

Mama Cookie Aapa Kuzaa Mpaka Baasi!



Mwanamama mkali kunano Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson Jujuman ‘Mama Cookie’, ameapa kuzaa mpaka baasi, huku akitanabaisha kuwa, kikubwa anachoangalia anazaa na nani, kwani hana mpango wa kuolewa.


Aunt ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, watu wengi wamekuwa wakishangazwa na yeye kubeba mimba na kutaka kumchunguza yeye na kusahau maisha yao ya kila siku.


“Kwenye akili yangu, sina mpango kabisa wa kuolewa. Mpango wangu ni kuzaa mpaka baasi, mpaka kieleweke maana nimeshaona wazi, nikibeba mimba watu wanakuwa bize kuchunguza nimeipata wapi, ni ya nani?


Basi inakuwa ni vurugu tupu, wakati mimba ni baraka na tabasamu kwa kila mwanamke,” amesema Aunt ambaye ni mama kijacho, huku akiwa na mtoto mwingine aliyezaa na Moze Iyobo ambaye ni dansa wa Lebo ya WCB

STORI:IMELDA MTEMA, IJUMAA

No comments

Powered by Blogger.