Header Ads

Header ADS

Maisha ya Samatta yalivyobadilika ghafla


Hatma ya Mbwana Samatta ndani ya kikosi cha Aston Villa bado haijajulikana,kufuatia timu hiyo kumsajili mshambuliaji mwingine Ollie Watkins kutoka timu ya Brentford


Samatta   aliyejiunga na  Aston Villa dirisha dogo la january , akitokea Genk ya Belgium ameshindwa kumshawish vyema kocha wake Dean Smith hadi kuamua kumsaka  mshambuliaji mwingine hali inayotoa tafsiri ya nafasi yake  ya kucheza au kusalia katika timu hiyo kuwa finyu

kumekuwa na tofauti kubwa  Mbwana  Samatta aliyecheza vilabu viwili tofauti katika soka la kulipwa TP Mazembe  na Krc Genk  ambapo alijitokeza kama mfungaji hodari  sana  kabla ya kujiunga na Aston Villa  ambapo hadi sasa ameshindwa kuonesha cheche zake pamoja na ukweli amekaa muda mchache ya miezi 8 hivi

Michezo 14  magoli  2  katika mashindano yote ukizingatia nafasi anayocheza ya mshambuliaji wa kati ni vigumu sana kumshawishi kocha yeyote  kuendelea na  mshambuliaji mwenye takwimu hizo.

WAPI  KUNAMFAA SAMATTA AKITOKA ASTON VILLA?

Samatta ana kipaji kikubwa anaweza kufunga kwa miguu  na kwa kichwa ,aina ya uchezaji wake umepata changamoto katika ligi ya  England kutokana na aina ya soka lao nguvu nyingi na kasi ya hali ya juu

Hivyo Samatta anaweza kucheza kokote duniani kusiko na aina ya uchezaji huo kama Uturuki , Denmark Sweden, Scotland na kungineko kwingi ambapo soka lake ni la maarifa zaidi na si nguvu zaidi

Ikitokea  Samatta anaaondoka  Aston Villa itapunguza  mashabiki wengi toka Tanzania waliokuwa wanaishabikia  Aston Villa kutokaa na uwepo wake , ikumbukwe muda mchache baada ya usajili wake kukamilika  akaunt zao za mitandao ya kijamii zilipanda kwa kasi kutokana na wafuasi wengi  wa Tanzania kutaka kupata taarifa za nahodha wao

No comments

Powered by Blogger.