Lipumba adai atakuwa Rais wa kwanza kupata Tuzo
Leo Septemba 7, 2020, Chama cha wananchi CUF kimezindua rasmi kampeni zake katika viwanja vya Sabasaba mkoani Mtwara, ambapo mgombea wa Urais kupitia chama hicho Prof Ibrahim Lipumba, amesema kama atachaguliwa atazingatia demokrasia na kuwa Rais wa kwanza atakayepata tuzo za Mo Ibrahim.
Profesa Lipumba amesema kuwa tuzo hizo, hutolewa kwa Marais ambao wanazingatia demokrasia na kuheshimu haki za binadamu na kudai kuwa hilo litakuwa lengo lake.
Akizungumza katika mkutano huo amesema Mikoa ya Kusini imeachwa solemba na CCM licha ya kubarikiwa na fukwe kubwa na zenye fursa za uwekezaji na kwamba uvuvi unaofanyika katika Bahari ni duni na usiotumia vyombo vya kisasa.
''Mikoa ya kusini ina bahati ya kuwa na fukwe kubwa,Mgombea mwenza wangu ni mwekezaji katika wa Hoteli za kitalii amepita Lindi na Mtwara anaiona Bahari, anaioina fursa za kuweza kutumia kuwa na biashara kubwa za kitalii'', amesema Profesa Lipumba.
''Kama kuna watu wana haki ya kuikataa CCM basi ni watu wa Kusini,mna Bahari lakini uvuvi unaofanyika ni uvuvi ulioduni na usio tumia vyombo vya kisasa, utastaajabu Tanzania tuna Bahari kubwa lakini eti tunavua Samaki wengi kwenye maji baridi kuliko baharini'', ameongeza.
No comments