Header Ads

Header ADS

Kinachondelea Msiba wa Mama wa P Funk




FAMILIA ya mtayarishaji wa muziki wa Bongo Fleva,  Paul Matthysse ‘P Funk Majani’,  ambao wamempoteza mama yao, Aunt Sheilah, juzi Septemba 8, nchini Uholanzi wakati akipatiwa matibabu, imetoa taarifa ya kinachoendelea kuhusu msiba huo.


 


Kaka wa marehemu Fadhili Kiholi amesema mipango ya mazishi inaendelea kufanywa, na kwa sasa msiba upo Kilosa mkoani Morogoro na ndipo atazikiwa baada ya kuurudisha mwili wa marehemu.


 


“Mpaka sasa hivi mwili bado upo Uholanzi, tunafanya michakato ya mwili kurejea hapa nchini.  Tutaondoka leo jioni na taratibu zote tunatarajia kuzifanya wiki ijayo.


 


“Marehemu alikuwa akiishi Tanzania na alienda Uholanzi mwezi wa tisa mwaka jana kama sehemu ya matibabu.  Huwa anaendaga mara kwa mara Uholanzi ila muda huu amekaa kidogo, pia mipango ya mazishi itafanyika Kilosa Morogoro kwenye ardhi aliyozaliwa,” amesema Kiholi.



No comments

Powered by Blogger.