Gigy Money Sirudiani na Mwanaume Nikiachana Naye
MREMBO asiyeishiwa vituko Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amesema kuwa katika maisha yake, hajawahi kurudiana na mwanaume aliyeachana naye.
Akipiga stori mbili tatu na Risasi Vibes, mwanamama huyo alisema hapa duniani kuna wanaume wengi wanaojua thamani ya mwanamke, hivyo haoni sababu msichana aanze kupata shida kwa mwanaume mmoja kila siku.
“Binafsi nikishaachana na mwanaume, ndiyo inakuwa imetoka hiyo, yaani kwa ufupi siwezi kurudiana na ex wangu zaidi ya mara mbili, wakati kuna wanaume wengine wazuri na wanaojua thamani ya mwanamke,” alisema Gigy
No comments