Header Ads

Header ADS

Faida saba(7) zitokanazo na juisi ya ukwaju


 Juisi ya ukwaju ina umuhumi sana katika miili yetu, pia tunda la ukwaju ni tunda lenye faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.

Zifuatazo ndizo faida zitokanazo na juisi ya ukwaju;
1. Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini ‘antioxidants’ ambavyo huzuia Saratani (cancer) kwa mtumiaji

2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile “carotentes”

3. Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo

4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni

5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa

6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)

7. Husaidia kurahisisha choo (laxative)

8.Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo

9.Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidond

10.Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)

Hizi Ndiyo Faida Kumi (10) Za Kula Ukwaju!
Unatakiwa ujaribu kuweka ukwaju karibu katika kila mlo wako kwa kila siku kwasababu ukwaju una faida nyingi kiafya ambazo hakika zitakufanya uwe na afya njema au kukuimarisha afya yako kiujumla

No comments

Powered by Blogger.