Esma: Najua Watu Wanafurahia Ndoa Yangu Kuvunjika
ULE usemi; ‘wataachana tu’ wakati wa kufungwa kwa ndoa ya dada wa mwanamuziki mkubwa barani Afrika, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, sosholaiti Esma Khan na Yahya Msizwa, unaendelea kutumika kueneza habari kuwa, ndoa hiyo imevunjika.
Lakini Esma amekanusha kuvunjika ndoa yake hiyo akisema; “Najua kuna watu wanafurahia sana kusikia ndoa yangu imevunjika!”
Esma ameweka wazi kuwa, kamwe hawezi kumuacha mumewe hata kama anamsifi a mke mwenzake. Mwanamama huyo anasema kuwa, yeye ameolewa ili akae kwenye ndoa na siyo kuachika.
Esma ameliambia Gazeti la IJUMAA WIKIENDA kuwa, anaona wiki nzima kwenye mitandao ya kijamii, watu wanamuongelea yeye na ndoa yake.
Amesema kuwa, hata kama mumewe ameandika maneno ya kummisi mke mwenzake, yeye haoni shida au angemmisi nani kama siyo mkewe, hivyo watu waache kumfuatilia kila kukicha. “Najua kuna watu wanafurahia kusikia ndoa yangu imevunjika.
“Watu hawakosi la kusema, hawaishiwi maneno, usipoolewa, watakusema na ukiolewa watakusema pia, hivyo naomba kuwaambia kuwa, sina mpango wa kuondoka kwenye ndoa yangu.
Wanaosubiri matarumbeta wanipigie, watasubiri sana na mume wangu kummisi mke mwenzangu, haina shida,” anasema Esma kufuatia kusambaa kwa taarifa za kuvunjika kwa ndoa yake iliyofungwa wiki kadhaa zilizopita. Wikiendi iliyopita, purukushani zilizuka kwenye mitandao ya kijamii, hasa wa Instagram, ikielezwa kuwa, wawili hao wameachana.
Chanzo cha taarifa hizo, ni kufuatia mume wa Esma kumposti mkewe mwingine na kumwambia kuwa, amemmisi huku Esma akiposti picha akiwa nyumbani kwake alipokuwa akiishi zamani, na kuandika kuwa amepamisi sana. Kufuatia posti hizo, wajumbe hawakutaka kuumiza vichwa, badala yake walikwenda moja kwa moja na kusema kuwa, ndoa hiyo iliyofungwa mwezi mmoja uliopita, imevunjika.
No comments