CAF Yampongeza CEO Mpya wa Simba...Wanaompinga Mlie tu
RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika, Ahmad Ahmad amemwandikia barua kumpongeza Mtendaji Mkuu (CEO) mpya wa simba, Barbara Gonzalez kwa uteuzi wake akimtakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya.
Barbara Gonzalez ni CEO wa kwanza mwanamke kuteuliwa katika klabu za Ligi Kuu Tanzania jambo ambalo limemgusa Rais huyo wa CAF.
Barbara anachukua mikoba ya aliyekuwa CEO wa timu ya Simba, Senzo Mbata ambaye alijiuzulu hivi karibuni na muda mfupi tu picha zilisambaa akiwa na viongozi wa Yanga ambao kwa sasa wamempa dili akiwa ni mshauri mkuu wa klabu hiyo yenye maskani yake pale Jangwani.
Kupitia barua ya pongezi Rais amendika kuwa ni furaha kwake kuona nafasi kubwa ya uongozi kwenye masuala ya michezo akipewa mwanamke jambo linaloweka usawa katika kazi na usawa kwa jinsia.
Pia ameongeza kuwa anakubali uwezo wa CEO mpya na kumtakia kila la kheri katika utendaji wake wa kazi.
Pia CEO huyo alipewa pongezi na Ubalozi wa Marekani wa Tanzania huku ukieleza kuwa umekuwa ukiunga kwa muda mrefu masuala ya wanawake katika uongozi na ndani ya uwanja.
No comments