Header Ads

Header ADS

VIDEO: Balozi wa Marekani Avua Barakoa Mbele ya Rais Magufuli, JPM Ampongeza Aangua Kicheko


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amepokea Hati za utambulisho za Mabalozi 2 walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa Tanzania.

Waliowasilisha hati hizo Ikulu Jijini DSM ni Dkt. Donald John Wright aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Marekani hapa nchini na Nguyen Nam Tien, aliyeteuliwa kuwa Balozi wa Vietnam hapa nchini.

Katika mazungumzo baada ya kupokea hati hizo, Rais Magufuli amewakaribisha Mabalozi hao hapa nchini na ameeleza kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati yake na nchi hizo.


Rais Magufuli amewaomba Mabalozi hao kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchini mwao kuja kuwekeza hapa nchini na kwamba Serikali itakuwa tayari wakati wowote kutoa ushirikiano kwao

No comments

Powered by Blogger.