Header Ads

Header ADS

Rekodi walizoweka Bayern ligi ya mabingwa ulaya


Bayern Munich wametwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa barani ulaya kwa mara ya sita baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya PSG katika mchezo wa fainali uliochezwa mjini Lisbon nchini ureno usiku wa jana.


Wachezaji wa Bayern Munich wakishangilia ubingwa wa ligi ya mabingwa ulaya baada ya kuifunga PSG 1-0 katika mchezo wa fainali

Bao la dakika ya 59 la Kingsley Coman lilitosha kuzima ndoto za PSG kutwaa ubingwa wa ulaya ambapo pia kikosi hicho kilikuwa kinacheza fainali ya kwanza ya michuano hii katika historia ya klabu hiyo

Hizi ni baadhi ya rekodi zilizowekwa na Bayern Munich baada ya mchezo wa fainali ya UEFA Champions League.

-Bayern Munich wameshinda mataji sita ya ulaya sawa na Liverpool, na ni Real Madrid ambao ni mabaingwa mara 13 na AC Milani ambao ni mabingwa mara 7 ndio wamechukua mara nyingi zaidi ya Byern Munic.

-The Bavarians imekua timu ya kwanza katika historia ya michuano ya klabu bingwa ulaya kushinda michezo yote 11 mfululizo mpaka wanatwaa ubingwa, wakiwa na wasani wa asilimia mia moja wa kushinda michezo yao.

-Bayern Munich imukuwa timu ya tatu kufikisha mabao 500 kwenye michuano hii, timu nyingine ni FC Barcelona waliofunga mabao 517 na Real Madrid wenye mabao 567 katika michuano hii.

-Kingsley Coman ni mchezaji wa tano raia wa Ufaransa kufunga katika mchezo wa Fainali ya Ligi ya mabingwa, wachezaji wengine raia wa ufaransa waliowahi kufunga kwenye fainali ya michuano hii ni Karim Benzema 2018, Zinedine Zidane 2002, Marcel Desailly 1994,na Basile Boli 1993.

-Robert Lewandowski amemaliza msimu akiwa mfungaji bora akiwa na jumla ya mabao 15. Ni kwa mara ya kwanza mfungaji bora hajatoka katika klabu ya Real Madrid au FC Barcelona tangu msimu wa 2007-08 ambapo Cristiano Ronaldo alimaliza kama kinara wa ufungaji akiwa na Manchester United.

-Kocha wa Bayern Hans-Dieter Flick ni kocha wa nne kutoka ujerumani kushinda ubingwa wa UEFA Champions League anaungana na makocha wengine raia wa Ujermani ambao wamewahi kutwaa ubingwa wa michuano hii ambao ni Ottmar Hitzfeld (1997 na 2001), Jupp Heynckes (1998 na 2013) na Jürgen Klopp (2019).

No comments

Powered by Blogger.