Mawe mawili ya dhahabu yenye thamani ya mamilioni ya fedha yapatikana Australia
Mawe mawili ya dhahabu yali
Brent Shannon na Ethan West walipata mawe hayo karibu na mji wa Tarnagulla jimbo la Victoria.
Mawe yao ya bahati yalioneshwa kwenye kipindi cha televisheni cha Aussie Gold Hunters, siku ya Alhamisi.
Wanaume hao walichimba ardhi katika eneo hilo na kutumia kifaa maalum kubaini mahali hapo kuna dhahabu.
“Huu bilashaka ni moja ya uvumbuzi muhimu,” Ethan West alisema, kwa mujibu wa kituo cha habari cha CNN. “Kupata mawe mawili makubwa mahali pamoja kwa siku ni jambo la kushangaza.”
Walipata mawe hayo yaliokuwa na uzani wa pamoja wa kilo 3.5 katika kipindi cha saa mbili akisaidiwa na baba yake West, kulingana na kituo cha Discovery ambacho hurusha kipindi hicho.Mawe hayo kwa pamoja yana uzani wa karibu kilo 3.5
Kipindi hicho ambacho pia hutangazwa nchini Uingereza, huwafuatilia wachimbaji madini katika migodi ya dhahabu katika baadhi ya maeneo ya vijijini Australia.
“Nakubali tulikuwa na bahati,” Bwana Shannon alisema katika kipindi cha televisheni cha Sunrise nchini Australia.
Bwana West amesema katika miaka yake minne ya uchimbaji wa kutafuta dhahabu “huenda amepata maelfu” ya vipande.
Kituo hicho cha Discovery pia kimesema watakaonunua mawe hayo huenda wakalipa 30% zaidi ya dhamani inayokadiriwa.
Mwaka 2019 mwanamume mmoja raia wa Australia alipata dhahabu ya kilo 1.4 iliyokadiriwa kuwa na thamani ya dola 69000 kwa kutumia mtambo wa kubaini mahali palipo na madini.
Uchimbaji dhahabu Australia ulianza miaka ya 1850, na unavailable kuwa sekta muhimu machine humo.
Mji wa Tarnagulla ulibuniwa wakati wa harakati za kutafuta dhahabu katika eneo la Victoria ambapo ulipata utajiri baada ya idadi kubwa ya wafanya bishara wa madini kuhamia hapo kutafuta mali zao kwa mujibu wa mtandao mmoja wa habari katika eneo hilo.
No comments