Header Ads

Header ADS

Kitilya na Wenzake Wakiri Makosa, Wahukumiwa Kulipa Faini Bil 1.5




ALIYEKUWA Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya, Shose Sinare, Sioi Solomon, Bedason Shallanda na Alfred Misana wamekiri makosa na wametakiwa kulipa TZS 1.5 bilioni kama fidia kwa kuisababishia hasara Serikali na kila mmoja kulipa faini shilingi milioni 1 ya mahakama au kwenda jela miezi 6, kutoka na kesi ya Uhujumu Uchumi iliyokuwa inawakabiri


 


Mashtaka yote 58 yalifutwa kwao na kubakiza shtaka moja la kuisababishia hasara Serikali. Kesi hii ilianza jana saa 11 na kuisha saa 2 usiku katika Mahakama ya Mafisadi.


 


Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani milioni 550 kwa Serikali ya Tanzania kutoka benki ya Standard ya Uingereza.


 


Aidha, wanadaiwa kula njama za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu ili waweze kujinufaisha wenyewe na washirika wao. Mawakili wa washtakiwa walikuwa ndg. Alex Mgongolwa na Jeremiah Mtobesya.


 





No comments

Powered by Blogger.