Rais Kenyatta Awataka WAKENYA Kutojilinganisha na Nchi Zinazoficha Taarifa za Corona
Rais Uhuru Kenyatta amesema Wakenya hawatakiwi kujilinganisha na Mataifa yasiyo na uhuru wa habari na ambayo yamekuwa hayatangazi taarifa za #CoronaVirus
Kauli yake inakuja kufuatia baadhi ya Wakenya mitandaoni kusema nchi hiyo inapaswa kulegeza masharti ya kudhibiti maambukizi kama Tanzania
Amesema #Kenya ni nchi ya kidemokrasia na vyombo vya habari vipo huru hivyo haiwezi kuficha taarifa. Nchi hiyo imerekodi visa 17,975 na vifo 285 huku wagonjwa 7,833 wakipona hadi sasa
No comments