Q Chief Afunguka Kumkataa Harmonize "Alikuwa na Nia Njema ila Nyuma yake Kuna Vitu Vilikuwa Vinaendelea Nikajikataa"
Msanii mkongwe wa BongoFleva Q Chief amesema yeye ndiyo aliamua kujikataa ili kutovunja heshima kwa msanii Harmonize baada ya kuwepo na maneno kuhusu kusaidiwa na msanii huyo.
Q Chief amesema Harmonize alikuwa na nia njema ya kumsaidia pia alipenda harakati ila kama mtu mzima alielewa kuna vitu vinaendelea hivyo aliamua kujikataa ili kutovunja heshima na thamani kwa kuamua kukaa kimya.
"Mdogo wangu alikuwa ana dhamira nzuri na maamuzi, alitaka kufanya kitu kwa ajili ya kaka yake na nilipenda harakati zake, ila kumbuka nyuma yake kuna taasisi na watu ambao wamemzunguka kwa hiyo kuna muda kukawa kuna vitu vinaendelea au kuongeleka nyuma yangu ambavyo sivielewi au sivijui, nikasema kutovunja heshima ya mtu aliyekupa thamani bora ukawa kimya nikajikataa" amesema Q Chief
No comments