Nasubiri Kumfumania Mke Wangu, Naombeni Ushauri
Waku habari za mchana,kama nilivyojieleza hapo juu,ni kwamba nilibahatika kuoa miaka 10 iliyopita iliyopita,tulipata sakrament ya ndoa takatifu tar.7/5/2011.pia katika ndoa yetu tumejaliwa kupata watoto 2.sasa kilichonifanya nije hapa jukwaani ni taarifa nilizozipata toka kwa jirani yangu ambae amenithibitishia kuwa mke wangu anatembea na mtu ambae pia ni jirani yetu kabisa.mke wangu huwa anashinda nyumbani akijishughulisha biashara ya kiduka tulichokifungua karibia mwaka sasa.pia mimi huwa nashinda kibaruani kwangu ambapo mara nyingi huwa nachelewa kurudi nyumbani kutokana na kabiashara kangu kanakonipatia riziki.huyu jirangu kanijulisha huwa wanatoka majira ya saa 1 jioni na kurudi sa 2:30 jioni kabla mimi sijarudi.baada ya kupata tarifa hizi nilijaribu kufanya uchunguzi na nimeanza kuona kuna ukweli juu ya jambo hili.juzi ilipofika saa 1:30 jioni nilimpigia simu kumuulizia jambo fulani nikasikia anaongea taratibu tofauti na siku nyingine,nikamuuliza umeshafunga duka?akanijibu ndio,nikamuuliza mbona mapema akasema kuna mkanda nimeupenda nauangalia..nikakata simu nikampigia yule jirani kumuuliza kama mke wangu yupo nyumbani akasema hayupo na ametoka na jamaa kama kawaida yake,kama huamini uje uone.nilitamani kwenda lakini nilishindwa kujua ni uamuzi gani nichukue kwa sababu,kwanza sikujua wamekwenda guest gani,huyo jamaa anausafiri hivyo wanauwezekano wa kwenda nje ya mji kidogo.nilijikaza sikumuuliza wala kumwonyesha dalili zozote za kufahamu mambo hayo machafu anayoyafanya mke wangu.hivyo naombeni ushauri wenu pindi nikiwafumania au kuwahi kurudi home na kumkosa mke wangu wakati amenijulisha yupo home..naombeni ushauri wenu ni uamuzi gani naweza kuchukua ukawa sahihi.
No comments