Mwanasheria wa Malawi Akataa Uteuzi wa Rais Mpya wa Kuwa Waziri wa Sheria...Adai Itaonekana Kama Kulipwa Fadhila
Mwanasheria wa Malawi, Mordecai Msiska amekataa uteuzi wa kuwa waziri wa Sheria na haki kwenye baraza la Rais Lazarus Chakwera.
Anasema itaonekana kama fadhila au thawabu baada ya kumsaidia Rais Chakwera kushinda kesi dhidi mpinzani wake (Mutharika), ambaye anadaiwa aliiba kura kwenye uchaguzi uliompa ushindi.
No comments