Morrisons, Tshishimbi na Jaffary Mohamed Walikuwa Hawapaswi Kuanza Kikosi cha Kwanza Jana- Bakari Malima
MCHEZAJI wa zamani wa Yanga, Bakari Malima maarufu kama Jembe Ulaya amesema kuwa Yanga ilifanya makosa makubwa kuwaanzisha kikosi cha kwanza wachezaji watatu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Julai 12 Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1. Ushindi huo unaipa nafasi Simba kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho.
Itakutana na Namungo FC inayonolewa na Hitimana Thiery, Agosti 2 Uwanja wa Nelson Mandela kwenye mchezo wa fainali.
Malima amesema:"Bernard Morrisons, Papy Tshishimbi na Jaffary Mohamed walikuwa hawapaswi kuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo kwa kuwa walishindwa kuumudu mchezo kipindi cha kwanza.
"Pia kitendo cha Morrison kushindwa kutulia ndani ya uwanja na kuondoka jumla bila kukaa benchi hii sio sawa kwani anaonekana hana nidhamu jambo ambalo halitakiwi katika timu inayotafuta mafanikio.
"Bado kuna nafasi ya Yanga kufanya marekebisho katika kile ambacho kimetokea, wafanye usajili mzuri na waepuke zile janjajanja kwenye usajili jambo ambalo litawapa matokeo mazuri kwenye mechi zao zinazofuata," alisema.
No comments