Bondia Mike Tyson Anajifua Kurudi ULINGONI Kuzichapa Ngumi Katika Umri wa Miaka 54
Mike Tyson ametangaza kurudi ulingoni, Septemba 12 atazichapa na Roy Jones Jr kwenye pambano ambalo litarushwa kupitia mtandao wa Triller.
Jana jumapili, Tyson ambaye ana umri wa miaka 54 alizungumza na kipindi cha First Take cha mtangazaji Max Killerman, alizungumzia pambano hilo ambalo linamrudisha Tyson ambaye alistaafu mchezo huo wa masumbwi tangu mwaka 2005.
Alipoulizwa kuhusu nini msukumo wa yeye kurejea ulingoni akiwa na umri huo mkubwa, Tyson alijibu "Kisa kwa sababu tuna miaka 54, haimaanishi kwamba inabidi tuanze kazi mpya na maisha yetu yanakuwa yamekwisha. Sio hivyo pale unapojisikia vizuri kama ambavyo mimi najisikia." alisema Mike Tyson akimtolea mfano Muhammad Ali aliyezichapa akiwa na umri wa miaka 47.
Katika kipindi cha hivi karibuni, bingwa huyo wa uzito wa juu amekuwa akiyatisha macho yetu kwa mazoezi makali na yenye nguvu.
No comments