Zari Kwa Afungua Moyo kwa Diamond "Lockdown ikiisha Tiffah na Nillan wataenda Tanzania kwa Baba yao"
Mjasiriamali na mzazi mwenza wa Diamond Platnumz , Zari the Boss lady amesema kwamba, hakuna shaka kuwa baada ya lockdown kuisha Nchini Afrika kusini , watoto wake ambao amezaa na Diamond Nillan na Tiffah watakuja Tanzania kuonana na baba yao , kwani Kama wazazi hawana Tofauti yoyote ile kwa hivi Sasa
Akizungumza kupitia Instagram Live, Zari amesema kuwa yeye na Diamond hawajarudiana kama watu wanavyodai, bali wameweka ukaribu ili kuwapa watoto wao malezi ya pamoja Kama wazazi
Zari amesema -"Sijarudiana na Diamond, yeye amejaliwa na mungu amemgusa, anafurahi sasa hivi amerejesha upendo kwa watoto wake.
Na Lockdown ikiisha watoto wake watakuja Tanzania kwasababu hakuna jambo lililo baya kati yetu"
No comments