Waziri Mpina Akosoa Operesheni ya Watendaji wake
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina ameitaka Bodi ya Maziwa kusitisha mara moja Operesheni ya kuharibu kwa kuyawekea Rangi na Mafuta ya Taa Maziwa yanayokutwa yakiwa nje ya Utaratibu wa kisheria, akiitaka Bodi hiyo kuandaa mikakati ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kukidhi matakwa ya kisheria.
Waziri Mpina amefikia uamuzi huo ikiwa ni mafanikio ya operesheni yake ya kustukiza iliyoanza majira ya saa 10 Alfajiri, akilenga kujionea uhalisia wa biashara hiyo, baada ya kufikiwa na taarifa za malalamiko ya wafanyabaishara wanaodai kutotendewa haki na maafisa kutoka Bodi ya maziwa.
No comments