Watumishi wa Jiji la Dar Es Salaam Wajionea Mradi wa Stendi Kuu ya Mabasi
Katika Kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma, Baadhi ya Watumishi wa Jiji la Dar es Salaam wametembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Stendi Kuu ya Kisasa ya Mabasi unaotekelezwa eneo la Mbezi Luisi kwa gharama ya shilingi billioni 50.9.
Wakizungumza baada ya kukagua Ujenzi wa Mradi huo wa Standi ya Mabasi Watumishi hao wakiongozwa na Afisa Utumishi wa Mkoa Dsm wamepongeza hatua zilizofikiwa huku wakitoa Wito kwa Makandarasi kuhakikisha wanakamilisha Mapema licha ya changamoto iliyojitokeza ya Kuchelewa kukamilika kutokana na Janga la Corona.
Wakati huo huo Watumishi hao wametoa Misaada mbalimbali ya Vyakula ,sabuni na Mafuta kwa Kituo cha kuwatunza wazee kilichopo Nunge Kigamboni Jijini Dsm
No comments