Header Ads

Header ADS

Watu 200,000 Waliodhuru Soko la Xinfadi Wanatafutwa Kufuatia Mlipuko Mpya wa Corona China



Wataalamu wa Afya wamejipanga kutafuta watu takriban 200,000 waliotembelea soko la Xinfadi ambalo limetajwa kuwa kitovu cha mlipuko mpya wa #COVID19 Jijini Beijing

Beijing imerekodi visa zaidi ya 70 tangu wiki iliyopita huku idadi kubwa ya maambukizi ikihusishwa na soko hilo kubwa la bidhaa mbalimbali za Vyakula

Imeelezwa kuwa Wataalamu wanafanya jitihada za kutafuta wote waliotembelea eneo hilo kuanzia Mei 30, na hadi sasa soko hilo pamoja na maeneo yapatayo 11 yaliyo jirani yamefungwa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Zhao Lijian amesema China imekuwa ikiwasiliana kwa karibu na Shirika la Afya (WHO) kuhusu mwenendo wa ugonjwa huo

No comments

Powered by Blogger.